
Pete ya Uchumba ya Ashlee Jenae bado haijapatikana, licha ya kwamba mwili wake umefikia familia yake. TMZ imebaini kuwa ingawa mwili wa Ashlee umerejeshwa kwa familia yake New Jersey, Marekani siku ya Ijumaa iliyopita na vitu vyake havijarudishwa.
Baba wa Ashlee, Harry Robinson, aliiambia TMZ kuwa familia haijapewa taarifa yoyote kuhusu lini vitu hivyo vitarejeshwa. Anaamini kuwa bado vinaendelea kushikiliwa kwa uchunguzi.
Harry alithibitisha kuwa familia imefanya uchunguzi huru wa mwili (autopsy), ingawa matokeo bado hayajakamilika. Kwa sasa, wanajiandaa kwa mazishi yatakayofanyika New Jersey wiki hii.

Kama ilivyoripotiwa awali, mamlaka zinasema kwamba Ashlee alikuwa na mzozo na mchumba wake, Joe McCann, muda mfupi kabla ya mwili wake kupatikana. Inaripotiwa kuwa wafanyakazi wa hoteli waliingilia kati na kuwagawa, kila mmoja akipewa chumba tofauti.
Ripoti za awali zinadai kuwa polisi walikuwa wanachunguza uwezekano wa kujidhuru, familia ya Ashlee imekanusha vikali nadharia hii. Wanasema kwamba Ashlee alikuwa ni mwangaza wa furaha na hakuwahi kuonyesha dalili na mawazo ya kujidhuru.

Familia pia imesema kuwa haijapata Ushirikiano kutoka kwa mchumba wa Ashlee, Joe McCann, tangu kifo cha binti yao. Hata hivyo, wanaendelea na juhudi za kupata video za kamera za usalama kutoka hoteli walikokuwa wakikaa, wakitumaini zitasaidia kueleza kilichotokea katika saa za mwisho za maisha ya Ashlee.
Katika harakati za kutafuta majibu, familia inaangalia uwezekano wa kusafiri hadi Tanzania ili kukutana na maafisa wa mamlaka kwa uso kwa uso, kama sehemu ya juhudi zao za kupata ukweli na haki.