×

Jaji Chande: Tume Haikutegemea Ushahidi Kutoka Kwa Polisi – Video

Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Jaji Mohamed Chande

Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Jaji Mohamed Chande amesema tume hiyo ilitegemea zaidi ushahidi kutoka kwa waathirika wa matukio ya vurugu na kwamba haikutegemea ushahidi mkubwa kutoka kwa polisi.

Jaji Chande ameendelea kusisitiza kuwa ndani ya siku 153 tume ilizopewa kufanya kazi, kila siku ilikutana ana kwa ana na mashahidi 40 na kufanya jumla ya watu 6,205 kutoa ushahidi ana kwa ana.

Jaji Chande, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo, Jumanne Aprili 28, 2026 alipozungumza na wahariri na waandishi wa habari.

Leave a Comment