×

Iraola Aibuka Mpinzani Mkubwa wa Carrick Mbio za Kuinoa Man United

Kocha wa AFC Bournemouth, Andoni Iraola, ameibuka kama mpinzani mkubwa wa Michael Carrick katika mbio za kuinoa Manchester United, kwa mujibu wa ripoti ya The Telegraph.

Inaelezwa kuwa United hawana haraka ya kufanya uamuzi wa kocha mkuu ajaye, licha ya Carrick kuipeleka timu karibu na nafasi za UEFA Champions League, wakiwa pointi mbili tu nyuma.

Carrick, ambaye ni kiungo wa zamani wa United, bado anaongoza katika orodha ya wagombea, huku akipata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wachezaji na benchi la ufundi ndani ya Carrington.

Hata hivyo, uongozi wa klabu unapanga kufanya mazungumzo na makocha wengine kabla ya kufikia uamuzi wa mwisho, huku wakitarajia kusubiri hadi mwisho wa msimu.

Ripoti hiyo inaongeza kuwa Iraola, anayetarajiwa kuondoka Bournemouth mwishoni mwa msimu, ndiye anayechukuliwa kama mpinzani mkubwa wa Carrick katika kinyang’anyiro hicho. Pia anahusishwa na nafasi ya ukocha katika Chelsea FC, pamoja na kuvutiwa kurejea katika klabu yake ya zamani Athletic Club nchini Hispania.

Leave a Comment