Kama Mwajiri Kinara nchini, tumedhamini na kushiriki maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika kitaifa mkoani Njombe, yakihusisha wafanyakazi kutoka sekta za umma, binafsi, taasisi na mashirika mbalimbali nchini.Katika maadhimisho hayo, tumepokea tuzo kama mdhamini wa kufanikisha maadhimisho haya, iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kupokelewa na Afisa Mkuu wetu wa Rasilimali Watu, Emmanuel Akonaay.
.jpeg)