
Muigizaji maarufu wa Hollywood, Cameron Diaz (53), amepata mtoto wake wa tatu pamoja na mume wake, mwanamuziki wa rock Benji Madden, katika taarifa ya kushtukiza iliyotolewa kupitia mitandao ya kijamii.
Benji Madden alitangaza habari hiyo kupitia Instagram, akieleza furaha kubwa ya familia yao na kumkaribisha mtoto wao wa kiume aliyepewa jina la Nautas Madden. Katika ujumbe wake, alisema familia yao iko na afya njema na wanafurahia maisha yao mapya ya uzazi.
Cameron Diaz hakuchapisha picha ya mtoto huyo, lakini alishiriki picha ya meli pamoja na maelezo ya jina “Nautas,” likimaanisha baharia, msafiri au mtu anayesafiri bila hofu ya yasiyojulikana. Pia alijibu ujumbe wa mume wake kwa emoji za upendo na nyota.
Wanandoa hao waliooana mwaka 2015 tayari wana watoto wengine wawili binti Raddix aliyezaliwa 2019 kupitia njia ya uzazi wa mpango, na mtoto wa kiume Cardinal aliyezaliwa 2024.

Habari hizi zinakuja wakati Cameron Diaz akiwa amerudi kwenye tasnia ya filamu baada ya mapumziko ya karibu miaka kumi, akishiriki kwenye filamu ya vichekesho vya giza Outcome pamoja na Keanu Reeves.
Akieleza uamuzi wake wa kujitenga kwa muda na uigizaji, Cameron alisema alitaka kurejea maisha yake binafsi na kujenga familia yake kwa utulivu, akisisitiza kuwa furaha yake ya kweli iko katika familia kuliko mafanikio ya kazi.
