
Dar es Salaam – Yas Tanzania imezindua rasmi applikesheni mpya ya “Yas App”, yenye lengo ya kubadilisha namna wateja wanavyopata huduma za mawasiliano na kuharakisha mwelekeo wa maisha ya kidijitali.
Yas App inatoa nafasi ya wateja kutumia na kufurahia Mtandao wa Viwango, kwan ni njia rahisi na shirikishi zaidi kwa Watanzania walio wengi wanaotegemea simu zao kwa shughuli za kila siku kuwasiliana, kufanya miamala na kushirikiana.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ikunda Ngowi, Meneja wa Vijana na Segimenti wa Yas Tanzania, alisema kuwa Yas App ni hatua muhimu katika safari ya mabadiliko ya kidijitali ya kampuni hyo.
“Kadri ulimwengu unavyoendelea kuwa wa kidigitali zaidi na Mahitaji ya wateja yanabadilika wakitaka huduma zilizo rahisi, za haraka na zinazobinafsishwa. Yas App inajibu mahitaji haya kwa kutoa urahisi, kasi na uzoefu shirikishi—ikiweka pamoja kila kitu ambacho mteja anahitaji katika sehemu moja,” alisema Ikunda.
Kupitia app hii, wateja wanaweza kusimamia kwa urahisi huduma zao za mawasiliano kama manunuzi ya muda wa maongezi, vifurushi, kulipa bili na kufuatilia matumizi kwa wakati halisi. Aidha, app hii inaunganisha huduma nyingine kama mikopo ya simu (device financing), usimamizi wa intaneti ya nyumbani (fiber), kuzuru (roaming) na vifurushi vya kimataifa.
Zaidi ya miamala, Yas App pia inafanya kazi kama kituo cha wateja kupata huduma za ziada kwa ajili ya maisha yao ya kila siku kama vile kuangalia maduka, kupata taarifa za habari, viwango vya ubadilishaji fedha na hali ya hewa.
“Haya ni mageuzi ya namna wateja wanavyoshirikiana nasi, kupitia Yas App tunamrahishia upatikanaji wa huduma, kudhibiti matumizi pamoja na nafasi za kujishindia zawadi kem kem ili waweze kushiriki na kufurahia uzoefu wa Mtandao wa Viwango,” aliongeza.
Applikesheni nii inawalenga zaidi vijana na watumiaji wa kidijitali, Yas inalenga kuhamasisha matumizi ya mara kwa mara ya app na kuifanya kuwa sehemu ya maisha ya kila siku kwa huduma za mawasiliano, mtindo wa maisha na zawadi.
App hii itaendelea kuboreshwa kulingana na maoni ya watumiaji, ikiwa ni sehemu ya mbinu ya maendeleo endelevu ili kuhakikisha inakidhi mahitaji ya Watanzania wa kisasa.