×

Mwili wa James Temba Wasili Moshi kwa Maziko Baada ya Mauaji ya Kikatili – Video

Mwili wa marehemu James Temba umefika leo Alhamisi Mei 7, 2026 katika Kijiji cha Mande, Kata ya Old Moshi Magharibi, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya maandalizi ya maziko.

Kwa mujibu wa taarifa za familia, mwili huo utazikwa katika makaburi ya familia nyumbani hapo, huku taratibu za maziko zikifanyika kulingana na mila na desturi za Wachaga. Baada ya kuwasili, mwili huo umeingizwa moja kwa moja ndani ya nyumba ya familia na kufuatiwa na ibada fupi ya kuaga.

James Temba alifariki katika tukio la mauaji lililosababisha huzuni na simanzi kwa familia, ndugu na wakazi wa eneo hilo.

Mazishi yake yanatarajiwa kufanyika katika mazingira ya maombolezo makubwa, huku jamii ikiendelea kutoa pole kwa familia iliyofikwa na msiba huo.

Leave a Comment