Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imemhukumu kunyongwa hadi kufa Abdalah Mussa maarufu Mr. Bluu, baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa makusudi Ezenia Kamana kwa kumkatakata vipande na kuvigawa katika mifuko nane ya salfeti na kuvitupa eneo la Ununio na Tegeta, Dar es Salaam.
Hukumu hiyo ilisomwa na Jaji Awamu Mbagwa wa Mahakama hiyo, baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 25 wa upande wa mashtaka, vielelezo 15, pamoja na utetezi wa mshtakiwa na sheria.
Huu ni uchambuzi wa kina wa ushahidi uliotumika kumtia hatiani Mr. Bluu ikiwemo jinsi alivyomchoma kisu marehemu wakiwa ndani ya gari.