×

Rais Samia Kuelekea Uganda Kuhudhuria Uapisho wa Museveni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Mei 12, 2026, anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Kampala, Uganda kuhudhuria sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni.

Taarifa ya Mei 11, 2026 iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari S. Machumu imeeleza ziara ya Rais Samia inaendeleza uhusiano wa kindugu na kihistoria kati ya Tanzania na Uganda, unaojengwa katika misingi ya umoja, mshikamano, ujirani mwema na ushirikiano wa kikanda.

Rais Museveni alichaguliwa kuiongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano katika Uchaguzi Mkuu wa Uganda uliofanyika tarehe 15 Januari, 2026.

Leave a Comment