×

TPLB Yamteua Yahaya Abushehe Kuwa Kaimu Ofisa Habari Mpya

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kumteua Yahaya Abushehe kuwa Kaimu Ofisa Habari wa TPLB akichukua nafasi ya Karim Boimanda ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Kwa mujibu wa taarifa ya leo Mei 14, 2026 iliyotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Cornel Barnabas uteuzi huo unaolenga kufanya mabadiliko kwenye kitengo cha Habari na Mawasiliano cha TPLB unaanza mara moja.

 

Leave a Comment