×

Trump Kuweka Historia kwa Saini Yake Kuwekwa Kwenye Dola za Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kuwa rais wa kwanza aliyepo madarakani kuweka saini yake kwenye noti za dola za Marekani, baada ya Wizara ya Fedha ya nchi hiyo kutangaza hatua hiyo mpya.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, saini ya Trump itaonekana sambamba na ile ya Waziri wa Fedha Scott Bessent, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 250 ya Marekani.

“Hakuna njia yenye nguvu zaidi ya kutambua mafanikio ya kihistoria ya taifa letu na Rais Donald J Trump kuliko kuweka jina lake kwenye noti za dola za Marekani,” amesema Bessent.

Kwa kawaida, noti za Marekani hubeba saini za maafisa wa Wizara ya Fedha pekee, hivyo hatua hiyo imeweka historia mpya nchini humo.

Taarifa hiyo imezua mjadala mkubwa nchini Marekani, huku baadhi wakiiunga mkono kama ishara ya heshima kwa rais huyo, na wengine wakikosoa hatua hiyo kwa kile wanachodai ni kuvunja utamaduni wa muda mrefu wa fedha za taifa hilo.

Leave a Comment