
Dar es Salaam-Tanzania, Mei 14, 2026: Kampuni ya Nishati ya Puma Tanzania imezindua rasmi programu yake ya kwanza nchini ya PRIS, iliyounganishwa kikamilifu na uaminifu kwa wateja wa mafuta. Hatua hii inaweka alama muhimu katika kuboresha huduma kwa wateja na kuendeleza ubunifu wa kidijitali ndani ya sketa ya nishati.
Kupitia mfumo wa PRIS, wateja watweza kujikusanyia pointi wanaponunua m,afuta,vilainishi, pamoja na bidhaa zinazopatikana katika maduka ya Puma Energy Tanzania. Point hiuzo zinaweza kutumika kupata zawadi mbalimbali ikiwemo bidhaa za matumizi ya nyumbani, chakula pamoja na punguzo la mafuta kupitia mtandao mpana wa washirika wa Puma Energy.

Uzinduzi wa programu hiyo pia unaunga mkono ajenda ya taifa ya mageuzi ya kidijitali kupitia Mfumo wa Kimkakati wa Uchumi wa Kidijitali (DESF) 2024–2034, unaolenga kuiweka Tanzania kama kitovu cha kidijitali katika ukanda kwa kuimarisha miundombinu, kupanua ujumuishaji wa kifedha na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Naibu Waziri wa Nishati Mheshimiwa Salome Makamba alisema :
“Napenda kuipongeza Kampuni ya Nishati ya Puma Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya nishati nchini, hususani katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora na zenye ufanisi kwa wananchi. Uzinduzi wa PRIS ni hatua muhimu inayokwenda sambamba na mwelekeo wa taifa wa kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidijitali katika utoaji wa huduma.”

“Kwa mtazamo wa serikali, ubunifu kama huu wa PRIS unaongeza thamani kwa wananchi kwa kuwawezesha kunufaika moja kwa moja na kila manunuzi yao kupitia mfumo wa pointi na zawadi. Mfumo huu unaimarisha ujumuishi wa kidijitali na kuchochea ushiriki wa wananchi katika uchumi wa kisasa.”
Lakini pia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nishati ya Puma Tanzania, Bi Fatma Abdallah alieleza kuwa:
“PRIS ni sehemu ya dhamira yetu ya kuwaweka wateja katikati ya kila tunachofanya. Tunaendelea kuwekeza katika suluhisho zinazotoa thamani halisi kwa Watanzania. Mfumo huu unabadilisha matumizi ya kila siku kuwa zawadi zenye manufaa, huku tukiunga mkono safari kubwa ya taifa, ya kuelekea maendeleo ya kidijitali na ukuaji wa uchumi.”
Programu hiyo imetengenezwa kwa kuzingatia urahisi na upatikanaji kwa kila mtumiaji. Wateja wanaweza kupakua app hiyo, kujisajili kwa kutumia namba yao ya simu na kuanza kujikusanyia pointi mara moja kwa kuonyesha QR Code wakati wa kufanya malipo. Baada ya kufikisha kiwango kinachohitajika cha pointi, wanaweza kuzitumia kupata bidhaa mbalimbali madukani au punguzo kwenye ununuzi wa mafuta siku zijazo.
Akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu mfumo huo, Meneja Mauzo wa Kampuni ya Nishati ya Puma Tanzania, Sulpis Mmasi:
“Programu ya PRIS imetengenezwa kwa kutumika kirahisi, kufikika kwa kila mtu na ina manufaa kwa wateja. Wateja wanajikusanyia pointi kila wanapoweka mafuta, na kununua bidhaa zingine za Puma, ambapo pointi hizo unaweza kuzitumia katika manunuzi yajayo kupitia mtandao unaoendelea kukua wa washirika wetu. Zaidi ya zawadi, app hii inatoa uzoefu wa kisasa na uwazi unaomwezesha mteja kufuatilia matumizi yake kwa urahisi.”
Uzinduzi wa PRIS pia unaendana na jitihada za Tanzania za kuelekea uchumi jumuishi wa kidijitali na matumizi makubwa ya mifumo isiyotumia fedha taslimu, kwa kuongeza urahisi, uwazi na usalama kwa watumiaji.
PRIS tayari imefanikiwa kutumika katika masoko mengine barani Afrika ambako Kampuni ya Nishati ya Puma inafanya shughuli zake, ikiwemo Zimbabwe, Malawi na Botswana, ambako imeonyesha kupokelewa vizuri na wateja pamoja na kuongeza ushiriki wao.
Kwa Kumalizia, Mkuu wa Idara ya Sheria na Mahusiano wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw. Emmanuel G. Bakilana, alsiwashukuru walke wote waliohudhuria katika hafla hiyo na kuwasisitiza kutumia App ya PRIS.
“Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wale wote mliohudhuria mahali hapa. Sisi kama kampuni ya Nishati ya Puma tumeweka kiapumbele cha kuhakikisha kuwa tunakuwa pamoja nanyi katika kila hatua. App hii haishii tu kutoa pointi, bali pia inakuonesha vituo vyetu vyote nchini, jambo ambalo litakurahisishia ujazaji wa mafuta kwa wateja wetu.”
Kuanzia leo, wateja wanaweza kupakua app ya PRIS, huku upanuzi wa huduma hiyo katika vituo vya Kampuni ya Puma nchini ukiendelea kwa kasi katika wiki zijazo.