
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameonesha masikitiko yake kufuatia tukio la kikatili la mauaji ya kijana James Temba, aliyeuawa na kukatwa kichwa huku baadhi ya viungo vyake vikidaiwa kuchukuliwa na wahusika wakiamini vitawapa utajiri.
Akizungumza katika kongamano la Wakala wa Vipimo, Chalamila amelaani vikali vitendo hivyo, akisisitiza kuwa ni ukatili usiokubalika katika jamii.
Aidha, amegusia suala la baadhi ya watu kudhulumu haki za wenzao, akionya dhidi ya tabia ya kufurahia mafanikio binafsi huku wengine wakiendelea kuteseka.
Amesisitiza umuhimu wa jamii kuzingatia haki, usawa na utu ili kujenga mazingira bora ya maisha kwa kila mwananchi.
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.