
Majina makubwa duniani ya michezo kama Cristiano Ronaldo, LeBron James, Lewis Hamilton na Roger Federer yameendelea kuthibitisha kuwa michezo ni moja ya njia kubwa zaidi za kutengeneza utajiri duniani.
Ripoti mpya iliyotolewa na Sportico imeorodhesha wanamichezo 50 walioingiza fedha nyingi zaidi katika historia ya michezo, ikihesabu mishahara, zawadi za mashindano pamoja na mikataba ya matangazo huku thamani ya fedha ikirekebishwa kulingana na mfumuko wa bei.
Bondia maarufu Floyd Mayweather ameingia kwenye orodha ya matajiri wakubwa wa michezo akiwa na mapato ya dola bilioni 1.57, huku akitajwa kuwa mmoja wa wanamichezo waliofaidika zaidi kupitia mapambano makubwa ya ngumi na mikataba ya matangazo.

Nyota wa tenisi Roger Federer ameingiza takriban dola bilioni 1.67 na kuwa mmoja wa wachezaji wa tenisi waliofanikiwa zaidi kifedha katika historia ya mchezo huo.
Kwa upande wa soka, David Beckham ametajwa kuwa mmoja wa wanasoka walioingiza fedha nyingi zaidi kuwahi kutokea, mafanikio yaliyotokana na kandanda pamoja na biashara na mikataba mikubwa ya matangazo hata baada ya kustaafu.

Orodha hiyo pia imeonyesha nguvu kubwa ya mchezo wa mpira wa kikapu huku mastaa kama Stephen Curry, Kevin Durant, Shaquille O’Neal na marehemu Kobe Bryant wakiingiza zaidi ya dola bilioni moja kila mmoja.
Katika mchezo wa Formula One, Michael Schumacher na Lewis Hamilton wameendelea kuwa miongoni mwa wanariadha waliotengeneza fedha nyingi zaidi kupitia mashindano ya magari duniani.
Ripoti hiyo imeonyesha namna michezo ya kisasa ilivyogeuka kuwa biashara kubwa inayoweza kubadilisha maisha ya wanamichezo kupitia mishahara mikubwa, udhamini na uwekezaji nje ya uwanja.
Wanamichezo Walioingiza Fedha Nyingi Zaidi Historia ya Michezo
- Michael Jordan — Dola Bilioni 4.15
- Tiger Woods — Dola Bilioni 2.79
- Cristiano Ronaldo — Dola Bilioni 2.23
- LeBron James — Dola Bilioni 1.88
- Lionel Messi — Dola Bilioni 1.85
- Arnold Palmer — Dola Bilioni 1.82
- Jack Nicklaus — Dola Bilioni 1.75
- David Beckham — Dola Bilioni 1.68
- Roger Federer — Dola Bilioni 1.67
- Floyd Mayweather — Dola Bilioni 1.57
- Phil Mickelson — Dola Bilioni 1.53
- Michael Schumacher — Dola Bilioni 1.42
- Shaquille O’Neal — Dola Bilioni 1.32
- Neymar — Dola Bilioni 1.24
- Greg Norman — Dola Bilioni 1.21
- Kevin Durant — Dola Bilioni 1.18
- Kobe Bryant — Dola Bilioni 1.13
- Lewis Hamilton — Dola Bilioni 1.08
- Stephen Curry — Dola Bilioni 1.06
- Mike Tyson — Dola Bilioni 1.00