×

Kenya Yashusha Bei ya Petroli na Dizeli Baada ya Mgomo wa Matatu Kenya

Siku moja baada ya mgomo wa usafiri wa umma wa matatu kutikisa maeneo mbalimbali nchini Kenya, Energy and Petroleum Regulatory Authority (EPRA) imetangaza kushuka kwa bei ya dizeli kwa KSh10.06 kwa lita huku bei ya mafuta ya taa ikipandishwa kwa KSh38.60 kwa lita.

Bei hizo mpya zimeanza kutumika leo Mei 19, 2026 na zinatarajiwa kudumu hadi Juni 14, 2026. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, petroli sasa itauzwa kwa KSh214.25 kwa lita, dizeli KSh232.86 na mafuta ya taa KSh191.38 kwa lita.

Tangazo hilo limekuja kufuatia mgomo wa matatu uliozua taharuki jana Jumatatu baada ya huduma nyingi za usafiri kusimama, hali iliyowaathiri maelfu ya wananchi waliokwama njiani wakielekea kazini na kwenye shughuli zao za kila siku.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya waendesha bodaboda pamoja na magari binafsi walipandisha nauli kwa kiwango kikubwa, jambo lililoongeza mzigo kwa wananchi waliokuwa wakitafuta usafiri mbadala.

Katika baadhi ya maeneo, wananchi walionekana wakifunga barabara na kuchoma matairi kupinga hali hiyo kabla ya polisi kuingilia kati na kudhibiti vurugu zilizokuwa zimeanza kujitokeza.

RAIS SAMIA AUNDA TUME MPYA ya UCHUNGUZI wa KIJINAI VURUGU za UCHAGUZI – JAJI SHABANI na WENGINE 3..

Leave a Comment