×

Bibi Wa Miaka 70 Ampongeza Rais Samia, Akitoa Ushuhuda Wa Daraja la JP Magufuli

Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega

Bibi Hellen Bugoye mwenye umri wa miaka 70 kutoka Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maboresho makubwa ya usafiri yaliyotokana na ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (zamani Kigongo-Busisi) linalounganisha Kigongo na Busisi.

Shuhuda za bibi huyo zimeelezwa bungeni jijini Dodoma leo Jumatano Mei 20, 2026 na Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Waziri Ulega amesema alipokea simu kutoka kwa Hellen Bugoye saa chache kabla ya kuingia bungeni, ambapo bibi huyo alimpa salamu za pongezi Rais Samia kutokana na manufaa yaliyopatikana baada ya kukamilika kwa daraja hilo.

Daraja la JP Magufuli (zamani Kigongo-Busisi) linalounganisha Kigongo na Busisi.

Kwa mujibu wa Ulega, bibi huyo amesema kwa miaka mingi wananchi walikuwa wakitumia muda mrefu kuvuka eneo la Kigongo-Busisi, lakini sasa safari hiyo imekuwa rahisi na ya haraka zaidi.

“Aliniambia tangu kukamilika kwa Daraja la JP Magufuli, unakunywa soda na kabla hujaimaliza tayari umeshafika upande wa pili,” amesema Ulega.

Amesema ushuhuda huo unaonesha namna Serikali ya Rais Samia inavyoendelea kugusa maisha ya wananchi kupitia uwekezaji katika miundombinu ya barabara na madaraja.

Waziri huyo ameeleza kuwa lengo la Serikali si kuongeza tu idadi ya kilometa za barabara, bali kuhakikisha miundombinu hiyo inarahisisha usafiri, inaunganisha wananchi na huduma muhimu pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

MELI KUBWA MBILI za MAFUTA za CHINA ZAPENYA HORMUZ BAADA ya KUKWAMA kwa MIEZI MIWILI….📍IRAN

Leave a Comment