×

Marekani Yaipa Iran Onyo Kali Kuhusu Hormuz, Yakataa Kutoza Ushuru

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio amesema makubaliano ya kidiplomasia kati ya Marekani na Iran hayatakuwa na uwezekano wa kufikiwa ikiwa Iran itaendelea na mpango wa kuweka mfumo wa kutoza ushuru kwa meli zinazopita katika Mlango wa Hormuz.

Rubio aliwaambia waandishi wa habari Alhamisi kuwa hakuna nchi duniani inayounga mkono hatua hiyo, akisisitiza kuwa mpango huo ni haramu kabisa na unatishia usalama wa dunia kutokana na umuhimu wa njia hiyo ya baharini katika usafirishaji wa mafuta na gesi.

Aidha, alisema kumekuwa na dalili za maendeleo katika mazungumzo ya kusitisha vita kati ya Marekani, Israel na Iran, ingawa alieleza kuwa mfumo wa uongozi wa Iran unaonekana kugawanyika jambo linalofanya mazungumzo kuwa magumu zaidi.

Rubio pia alieleza matumaini yake kuhusu ziara ya mkuu wa jeshi la Pakistan kwenda Tehran, akiamini inaweza kusaidia juhudi za kidiplomasia kumaliza mzozo huo.

Wakati huo huo, aliikosoa NATO kwa kile alichodai ni kushindwa kuunga mkono kampeni ya Marekani dhidi ya Iran, akisema Marekani haikuridhishwa na msimamo wa baadhi ya washirika wake ndani ya muungano huo.

MOJTABA ATEMA CHECHE – ADAI ni HAKI ya IRAN KUITUMIA URANIUM – “HAIPELEKWI MAREKANI”.

Leave a Comment