
Malkia wa muziki wa pop, Madonna (67), ameendelea kuwavutia mashabiki wake baada ya kuonekana akiwa na mwonekano wa kuvutia katika picha mpya iliyosambazwa kupitia Instagram.
Madonna mwenye umri wa miaka 67 alionekana akiwa amekaa kwenye sofa ya ngozi nyeusi ndani ya ukumbi wenye mwanga hafifu wa mishumaa na mandhari ya usiku wa Manhattan. Katika picha hiyo, staa huyo alikuwa amevaa gauni la pinki hafifu, jeupe pamoja na sleeves za rangi ya silver zilizong’aa.
Hata hivyo, kilichowavutia zaidi mashabiki ni glovusi zake za ngozi za rangi ya purple zilizokuwa na muundo wa kipekee unaoacha sehemu ya vidole wazi. Wengi wanaamini kuwa uchaguzi huo wa mavazi si wa kawaida bali ni sehemu ya ujumbe maalum kuelekea uzinduzi wa albamu yake mpya ya 15 inayojulikana kama Confessions II, inayotarajiwa kutoka Julai 3.

Mashabiki wa Madonna wamekuwa wakichambua kila picha na muonekano wake kwa karibu wakiamini kuwa staa huyo hutumia fashion kuwasilisha ujumbe wa kisanii kabla ya kuachia kazi zake mpya.
Kwa miaka mingi, Madonna amekuwa akitumia mitindo ya mavazi, picha na accessories kama sehemu ya simulizi la muziki wake, jambo lililomfanya kubaki kuwa mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa duniani.

