×

Dkt. Mwigulu Aondoka Nchini Kumwakilisha Rais Samia Congo Brazzaville

WAZIRI MKUU wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameondoka nchini leo Jumatatu Mei 25, 2026 kuelekea Brazzaville, Jamhuri ya Kongo kwa ajili ya kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Mkutano huo mkubwa wa kimataifa unatarajiwa kufanyika Mei 26 hadi 27, 2026 katika ukumbi wa kimataifa wa Kintele uliopo jijini Brazzaville, huku ukitarajiwa kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa serikali, taasisi za fedha pamoja na wawekezaji kutoka mataifa tofauti duniani.

Katika mkutano huo, viongozi wa Afrika na washirika wa maendeleo watajadili masuala muhimu yanayohusu ukuaji wa uchumi wa bara la Afrika, upatikanaji wa rasilimali za kifedha pamoja na mbinu za kukabiliana na changamoto za kiuchumi zinazoendelea kuikabili dunia.

Zaidi ya wajumbe 3,000 wanatarajiwa kushiriki mkutano huo, wakiwemo Mawaziri wa Fedha, Magavana wa Benki Kuu, wafanyabiashara, taasisi za kifedha, wawekezaji pamoja na washirika wa maendeleo kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo unatajwa kuwa sehemu ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na taasisi za maendeleo pamoja na kutafuta fursa mpya za uwekezaji na maendeleo kwa taifa.

JAJI MANYOTA – ”HAMAHAMA KISIASA – MSIGWA na SELASINI WAMEFELI PAKUBWA”…

Leave a Comment