×

Rapa Marekani Pop Smoke Auawa kwa Kupigwa Risasi

MSANII wa Hip-hop  nchini Marekani, Bashar Barakah Jackson maarufu Pop Smoke (20), amefariki baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana waliomvamia nyumbani kwake.

 

Polisi  wamethibitisha  tukio hilo na hadi sasa hakuna aliyekamatwa.

 

Smoke aliuawa jana Jumatano Februari 19, 2020,  katika mazingira  yanayooenaka kama uvamizi akiwa nyumbani kwake mjini Hollywood Hills.

 

Mwanamuziki huyo amewahi kufanya kazi na Nick Minaj  na Travis Scott na alikuwa anapewa nafasi ya kufanya vizuri katika muziki wake.

Leave a Comment