×

Morocco Kukipiga dhidi ya Burundi leo, Kuelekea Kombe la Dunia 2026

Leo Mei 26, 2026 saa 19:00 kwa saa za Morocco, Uwanja wa Stade de Marrakech utakuwa mwenyeji wa mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Morocco na Burundi.

Mechi hii haijalishi kwa pointi, lakini ni muhimu kwa Morocco kujenga kasi kabla ya Kombe la Dunia 2026. Kwa upande mwingine, Burundi wanaiona kama fursa ya kujipima dhidi ya timu kubwa barani Afrika.

Mechi itachezwa bila mashabiki jambo ambalo linaondoa shinikizo la sauti za watazamaji. unaoweza kupunguza kasi ya mchezo. Kwa sababu hiyo, makocha wote watapaswa kuzingatia ubadilishanaji wa wachezaji mara kwa mara ili kuepusha uchovu mwingi.Morocco ina safu ya ulinzi imara ambayo haijafungwa katika mechi 6 za nyumbani mfululizo. Hata hivyo, tatizo lao kubwa ni kukosa mshambuliaji anayetia hofu kiwango cha kimataifa baada ya Youssef En-Nesyri kupungua kasi.

Mechi ya leo itatumika kuwajaribu wachezaji wapya kama Ayoub Bouaddi na kumalizia nafasi za mabao jambo walioshindwa kukifanya kwenye fainali ya AFCON 2025.

Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Burundi ni timu inayojihami kwa nidhamu, na katika kufuzu kwa AFCON mara chache walifungwa kwa tofauti kubwa. Ushindi wao wa mabao 4-0 dhidi ya Chad Machi ulionyesha uwezo wa mashambulizi ya haraka.

Hata hivyo, kukosa wachezaji waliokomaa katika ligi kuu za Ulaya ni changamoto yao kubwa, hasa wanapokabiliwa na kasi ya wachezaji wa Morocco nyumbani kwao.Kutokana na tofauti ya viwango na rekodi ya Morocco nyumbani, tunatarajia Morocco kushinda, Kwa Burundi, kufungwa kwa tofauti chini ya mabao mawili utakuwa ushindi wao wa kimaadili. Mechi hii ni darasa la kujenga kujiamini kwa Morocco kabla ya safari ndefu ya Dunia.

Leave a Comment