×

Video: Wimbo wa Ozalima wa Mbosso Wabeba Hisia Nzito za Mapenzi

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Mbosso

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Mbosso, ameendelea kuwavutia mashabiki kupitia wimbo wake mpya “Ozalima” ambao umeibua mjadala mkubwa kutokana na jina na ujumbe wake wa kipekee wa kimapenzi.

Neno “Ozalima” limetokana na lugha ya Hindi-Urdu likiwa na maana ya “mtesi”, “mkatili” au “anayetesha mateso”. Hata hivyo, katika wimbo huo, neno hilo limetumika kwa mtazamo wa kimapenzi na si kwa ubaya.

Kupitia mashairi yake, Mbosso anaeleza jinsi uzuri wa mwanamke anayempenda unavyomchanganya akili na kumfanya ashindwe kupata utulivu. Anafafanua kuwa mapenzi hayo yana uzito mkubwa moyoni mwake kiasi cha kuhisi kama amebeba mzigo mzito wa hisia.

Katika baadhi ya mistari ya wimbo huo, Mbosso anatumia lugha ya mafumbo kuonesha namna anavyotaka kumlinda mpenzi wake dhidi ya watu wengine wanaoweza kuvutiwa naye. Msanii huyo anasema yupo tayari kuweka ulinzi mkali, ikiwa ni ishara ya wivu wa kimapenzi na upendo mkubwa alionao.

Mashabiki wengi wamepongeza ubunifu wa mashairi ya “Ozalima”, wakieleza kuwa wimbo huo umebeba hisia halisi za mapenzi pamoja na mtindo tofauti wa uandishi wa muziki.

Video rasmi ya wimbo huo tayari imeanza kufanya vizuri kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki na mitandao ya kijamii huku wengi wakivutiwa na ujumbe wake wa kipekee.

Leave a Comment