×

Mechi za Tanzania Dhidi ya Uganda na Rwanda Zafutwa Morocco

Mechi mbili za kimataifa za kirafiki za timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars dhidi ya Rwanda na Uganda zilizokuwa zimepangwa kufanyika Juni 5 na Juni 9 mwaka huu nchini Morocco, zimefutwa rasmi.

Kwa mujibu wa taarifa, uamuzi huo umechukuliwa na mamlaka za Morocco kutokana na tishio la ugonjwa wa Ebola, hatua iliyolenga kuimarisha tahadhari za afya na usalama wa wageni na wakazi.

Awali, Taifa Stars ilitarajiwa kucheza mchezo wa kwanza Juni 5 dhidi ya Uganda na kisha Juni 9 dhidi ya Rwanda, yote yakipangwa kuchezwa jijini Marrakech, Morocco kama sehemu ya maandalizi ya mechi za kimataifa.

Leave a Comment