×

Polisi Zanzibar Watoa Hitimisho la Kifo cha Ashlee Robinson, Uchunguzi Wabaini Alijinyonga

Jeshi la Polisi Zanzibar kupitia Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai limetoa taarifa ya uchunguzi kuhusu kifo cha mwanaharakati wa mitandao ya kijamii kutoka Marekani, Ashlee Jenae Robinson, kikieleza kuwa alifariki baada ya kujinyonga kutokana na msongo wa mawazo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Juni 4, 2026 na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Zuberi Chembera, tukio hilo lilitokea Aprili 8, 2026 katika Hoteli ya Zuri iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja akiwa na mchumba wake Joseph McCann. Ashlee alifariki dunia siku iliyofuata akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Ampolla Mkoa wa Mjini Magharibi.

Polisi wamesema uchunguzi uliofanywa kupitia ushahidi wa mashahidi pamoja na uchambuzi wa mawasiliano ya simu umeonyesha kuwa marehemu alikuwa akipitia changamoto za msongo wa mawazo kwa muda.

Taarifa hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa sintofahamu na mijadala kwenye mitandao ya kijamii iliyodai kuwa mwanaharakati huyo aliuawa na mchumba wake, jambo lililopelekea polisi kumshikilia Joseph McCann kwa uchunguzi zaidi kabla ya hitimisho la uchunguzi kutolewa.

Leave a Comment