Rais Samia Aandika Historia Atunukiwa Udaktari wa Heshima Moscow (Picha +Video)
Global Publishers June 4, 2026 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University) kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Profesa Oleg Yastrebov kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo Moscow nchini Urusi, tarehe 04 Juni, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Peoples’ Friendship University of Russia katika hafla iliyofanyika jijini Moscow, nchini Russia Juni 4, 2026.
Shahada hiyo ilitolewa na Mkuu wa chuo hicho, Oleg Yastrebov, kwa kutambua mchango wa Rais Samia katika mageuzi ya sekta ya elimu, kuimarisha diplomasia ya Tanzania pamoja na kuinua hadhi ya nchi kimataifa kupitia sekta mbalimbali ikiwemo utalii.
Tuzo hiyo pia imeelezwa kuwa ni ishara ya kuthamini juhudi zake katika kuendeleza ushirikiano wa kimataifa na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na mataifa mengine duniani.
Rais Samia atunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University) Moscow nchini Urusi. Rais Samia akihutubia viongozi wa Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University), Wanafunzi wa Chuo hicho, wageni mbalimbali baada ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa).