×

Wabunge wa Republican Wawaunga Mkono Democrats Kumpinga Trump

Rais Donald Trump

Bunge la Wawakilishi nchini Marekani limepitisha azimio la kupunguza mamlaka ya Rais Donald Trump katika vita dhidi ya Iran, hatua inayotajwa kuwa pigo kubwa kwa utawala wake kuhusu namna ulivyoshughulikia mgogoro huo uliodumu kwa miezi mitatu.

Azimio hilo limepitishwa kwa kura 215 dhidi ya 208, huku wabunge wanne wa chama cha Republican wakijiunga na Democrats kuunga mkono hatua hiyo. Ingawa azimio hilo halina nguvu ya kisheria moja kwa moja, limetuma ujumbe mzito kwa Ikulu ya Marekani kuhusu hali ya wasiwasi iliyopo bungeni.

Azimio hilo linamtaka Trump kusitisha matumizi ya jeshi la Marekani dhidi ya Iran bila idhini rasmi ya Congress ya kutangaza vita au matumizi ya nguvu za kijeshi.

Baada ya kura hiyo, mbunge wa Democrat Gregory Meeks alisema Congress imeamua “imetosha,” akisisitiza kuwa ni wakati wa kumaliza vita hivyo na wananchi kuelezwa sababu ya Marekani kuingia kwenye mgogoro huo.

Hata hivyo, Spika wa Bunge Mike Johnson alipinga azimio hilo akisema linaweza kuondoa uwezo wa rais kufanya mazungumzo muhimu ya kidiplomasia wakati huu mgumu.

MCHUNGAJI MSIGWA ALIPUKA – “WAKATI wa KINANA na NAPE WALIWEKA WAZI MAWAZIRI WENGINE ni MIZIGO”….

Leave a Comment