
Kim Kardashian ameonekana akimpa sapoti mpenzi wake Lewis Hamilton wakati wa mazoezi ya kufuzu kuelekea Monaco Grand Prix 2026 iliyofanyika katika Circuit de Monaco, Monte-Carlo.
Kim, mwenye umri wa miaka 45, alihudhuria tukio hilo akiwa pamoja na dada yake Khloé Kardashian pamoja na rafiki wa karibu wa familia Simon Huck. Kabla ya mbio hizo, inaripotiwa kuwa walifika Monaco kwa safari ya boti siku moja kabla ya tukio hilo kubwa la mashindano ya Formula 1.

Katika siku ya tukio, Kim alivutia macho ya wengi akiwa amevaa vazi la Gucci la rangi nyeusi (black lace bodysuit) pamoja na jeans na viatu virefu (black heels). Alionekana akiwa katika eneo la Ferrari akimshuhudia Hamilton akijiandaa kushindana akiwa na timu ya Ferrari.

Lewis Hamilton, mwenye umri wa miaka 41, anashiriki msimu wa Formula 1 wa 2026 akiwa na Ferrari, na uwepo wa Kim umekuwa sapoti kubwa kwake katika mashindano ya F1.
Uhusiano wao umeendelea kuvuta hisia za mashabiki duniani, huku kuonekana kwao Monaco kukionekana kama uthibitisho zaidi wa uhusiano wao kuendelea kuwa wazi mbele ya umma.