
Zikiwa zimebaki saa kadhaa Kombe la Dunia 2026 kuanza, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Ronald Shelukindo leo amesema lengo lao ni kuhakikisha kila mtu anapata fursa ya kushuhudia michuano hiyo mikubwa ya soka duniani. Kutokana na hilo, kwa kipindi hiki dekoda za DStv zinauzwa kwa Tsh 15,000 tu, huku kifurushi kitakachoonesha michuano hiyo kikiuzwa kwa Tsh 27,500, ambapo watazamaji watapata nafasi ya kufuatilia mechi zote 104 za mashindano hayo.
Michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu inatarajiwa kuwa na msisimuko wa kipekee kutokana na ongezeko la timu shiriki kutoka 32 hadi 48, hatua ambayo imeongeza idadi ya mechi na ushindani kwa kiasi kikubwa. Kwa mara ya kwanza katika historia, Afrika itawakilishwa na timu 10, jambo linaloongeza matumaini kwa mashabiki wa bara hilo kuona mataifa yao yakifanya vizuri zaidi kwenye jukwaa la dunia.

Aidha, maboresho ya teknolojia ya utangazaji yanatarajiwa kuwapa watazamaji uzoefu wa kipekee zaidi, huku mashabiki wakipata fursa ya kufuatilia kila hatua ya michuano hiyo kuanzia mechi za makundi hadi fainali. Kuongezeka kwa idadi ya timu kunamaanisha mechi nyingi zaidi, ushindani mkubwa zaidi na nafasi pana kwa mataifa yanayoibukia kuonyesha uwezo wao kwenye jukwaa la dunia.
Hali hiyo inatarajiwa kuongeza hamasa kwa mashabiki wa soka barani Afrika na duniani kote, ambao watakuwa na matumaini ya kuona timu zao zikifanya vizuri na kuweka historia mpya katika moja ya mashindano makubwa zaidi ya michezo duniani.