
Klabu ya Yanga imetangaza uteuzi wa Kamati ya Uchaguzi itakayosimamia mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo, huku Adv. Malangwe Mchungahela akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 13, 2026 na Idara ya Mawasiliano ya Yanga SC, Adv. Samuel Mangesho ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
Wajumbe wengine walioteuliwa katika Kamati ya Uchaguzi ni Adv. Godfrey Mapunda, Adv. Nelson Mwakingwe pamoja na Yassir Nassor.
Uteuzi huo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya Yanga SC ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo.
Hatua hiyo inaashiria mwanzo wa maandalizi rasmi ya uchaguzi, huku mashabiki na wanachama wa Yanga wakisubiri ratiba na taratibu nyingine zitakazotolewa na Kamati ya Uchaguzi katika kipindi kijacho.
