
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs imetangaza nafasi 95 za kazi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo, kupitia tangazo lenye kumbukumbu Kumb. Na. JA.9/16/01/41 la tarehe 13 Juni 2026.
Nafasi hizo zinahusisha kada mbalimbali za afya, fedha na ukaguzi, ikiwa ni pamoja na wataalamu wa maabara, dawa, radiolojia, uhasibu, ukaguzi wa ndani, pamoja na wauguzi na madaktari wa meno.
FUNGUA HAPA >>NAFASI ZA KAZI MDAs NA LGAs
Baadhi ya nafasi zilizotangazwa ni:
- Mteknolojia Msaidizi Maabara (10 nafasi)
- Mteknolojia Msaidizi – Dawa (10 nafasi)
- Mteknolojia Msaidizi – Radiolojia (10 nafasi)
- Radiography Technologist II (10 nafasi)
- Mkaguzi wa Ndani Daraja II (15 nafasi)
- Mhasibu Daraja II (10 nafasi)
- Tabibu wa Kinywa na Meno (10 nafasi)
- Daktari wa Upasuaji wa Kinywa na Meno (10 nafasi)
- Muuguzi II (10 nafasi)
Masharti ya jumla
Waombaji wanatakiwa kuwa raia wa Tanzania, wasiozidi umri wa miaka 45, na kuwasilisha vyeti sahihi vilivyothibitishwa. Aidha, maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa ajira kupitia:
👉 https://portal.ajira.go.tz/
Sekretarieti imesisitiza kuwa maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu hayatazingatiwa, na mwisho wa kutuma maombi ni 26 Juni 2026.
FUNGUA HAPA >>NAFASI ZA KAZI MDAs NA LGAs