×

Simba Yatinga Fainali Kombe la Shirikisho Baada Ya Kuwafunga Coastal Union 4-0 Arusha

Simba leo Juni 20, 2026 wamefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB (FA Cup) baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Simba walionyesha ubabe wao kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo, wakitawala mchezo na kutumia vizuri nafasi walizopata.

Kwa ushindi huo, Simba sasa wanasubiri mshindi kati ya vigogo wengine wawili wa Ligi Kuu, Young Africans SC na Azam FC, watakaokutana kwenye nusu fainali ya pili kuamua nani atakutana na Mnyama kwenye fainali.

Mashabiki wa soka nchini sasa wanatarajia fainali yenye mvuto mkubwa, hasa kutokana na ubora wa timu zilizobaki katika mashindano hayo ya CRDB FA Cup.

MATOKEO KAMILI (FT)

Simba SC 4-0 Coastal Union

⚽ 20’ — Gueye
⚽ 55’ — Kibabage
⚽ 75’ — De Reuck (penati)
⚽ 78’ — Chama

Leave a Comment