×

Wafanyabiashara Sita wa Bangi Wafungwa Miaka 30 Wilaya ya Mufindi, Iringa – Video

Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa, Juni 19, 2026, imewahukumu watuhumiwa sita baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mbalimbali yanayohusiana na dawa za kulevya aina ya bangi.

Katika hukumu hiyo, Dorice George Mvemba ametiwa hatiani kwa makosa mawili ya kusafirisha bangi yenye uzito wa kilogramu 34.949 na gramu 132.14, na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kila kosa.

Watuhumiwa wengine watatu, ambao ni Apolonia Ramadhan Chambo, David Daima Sanga na Khadija Yekonia Mahenge, wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha bangi yenye uzito wa kilogramu 34.949.

Aidha, Oriva Mwaigaga Saimon amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kusafirisha bangi yenye uzito wa gramu 132.24.

Kwa upande mwingine, Yacobo, Oriva Mwaigaga Saimon na Joraham Mhesa wamehukumiwa kulipa faini ya shilingi milioni moja kila mmoja au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na bangi yenye uzito wa gramu 46.22.

Leave a Comment