
Yumna Mmanga Omar, Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha makundi ya Watu wenye Ulemavu kutoka Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), leo Juni 25, 2026, amesimama bungeni na kumuuliza swali Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba.
Katika swali lake, Yumna amejikita kuhoji kuhusu maendeleo ya sekta ya michezo kwa watu wenye ulemavu nchini.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba ameeleza mikakati mbalimbali ambayo Serikali imeweka ili kuimarisha na kuendeleza michezo kwa watu wenye ulemavu, akisisitiza dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kundi hilo linapata fursa sawa za kushiriki na kufanya vizuri katika michezo.