×

Q Chief Afunga Ndoa, Mke Afunguka Jinsi Walivyokutana Kwa Mara ya Kwanza

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Aboubakar Katwila almaarufu Q Chief, jana alifunga ndoa, shughuli iliyofanyika Mwanagati, Kitunda jijini Dar es Salaam.

Msikilize mkewe alichokisema, ikiwemo jinsi walivyokutana kwa mara ya kwanza na kilichoendelea mpaka walipofunga ndoa.

Mwanamama huyo ameelezea kuwa kwa mara ya kwanza alikutana na Q Chief hospitali kama anavyokutana na wagonjwa wengine na akamhudumia lakini hakuwa amefikiria kwamba anaweza kumpenda na mwisho wakawa mume na mke.

Akizungumza na Global TV, mwanamama huyo amesema amempenda kama Aboubakar na siyo Q Chief na kuwaahidi mashabiki wa msanii huyo mkongwe watarajie mabadiliko makubwa kwenye maisha yake na kazi zake.

Leave a Comment