×

Video: Aliyedaiwa Kulima Ekari 2 za Bangi na Mwenzake Wafikishwa Mahakamani

Watu wawili, Madumuka Zilihona (60) na Mawazo Manisha (50), wakazi wa Kijiji cha Busekeseke wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Sengerema wakikabiliwa na mashtaka yanayohusiana na dawa za kulevya.

Madumuka anadaiwa kukutwa na dawa za kulevya pamoja na kulima ekari mbili za bangi. Hakuruhusiwa kujibu shtaka la kwanza kwa kuwa ni la uhujumu uchumi lisilo na dhamana.

Kwa upande wake, Mawazo Manisha anadaiwa kukutwa na kilo 13.50 za bangi. Alikana shtaka hilo lakini alishindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama.

Kesi zote zimeahirishwa hadi Julai 2, 2026, huku washtakiwa wote wakirudishwa rumande.

 

Leave a Comment