×

Cardi B Aacha Historia BET 2026, Afanya Shoo Ya Kibabe Jukwaani

Rapa nyota wa Marekani, Cardi B, amevutia dunia baada ya kutoa onyesho kali katika Tuzo za BET  2026, akitumbuiza nyimbo kutoka albamu yake mpya “Am I the Drama?” kwenye jukwaa la Peacock Theater jijini Los Angeles usiku wa kuamia leo Juni 29, 2026.

Cardi B alitokea kwa mtindo wa kipekee akianza onyesho lake juu ya pikipiki kabla ya kuendelea na mfululizo wa nyimbo zake maarufu, katika show iliyosheheni choreography kali na mwonekano wa kisasa wa jukwaani.

Kwa mujibu wa taarifa za hafla hiyo, Cardi B aliimba nyimbo kadhaa kutoka albamu yake mpya ambayo imekuwa ikiongoza chati mbalimbali za muziki duniani, huku mashabiki wakifurahia kila sekunde ya onyesho lake lililojaa ubunifu.

Rapa huyo pia alikuwa miongoni mwa wasanii walioteuliwa katika vipengele vingi vya tuzo hizo za mwaka huu, akithibitisha nafasi yake kama mmoja wa wasanii wakubwa wa hip hop duniani.

BET Awards 2026 zimeendelea kuonyesha ushindani mkali na ubunifu mkubwa kutoka kwa wasanii mbalimbali, lakini onyesho la Cardi B limechukuliwa kama moja ya highlight kubwa ya usiku huo wa burudani.

Leave a Comment