
Kamati ya Uchaguzi ya Yanga SC imetangaza orodha ya wanachama waliochukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu hiyo kuelekea uchaguzi ujao.
Kwa mujibu wa orodha hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Adv. Malangwe A. Mshungahale, nafasi ya Rais ina mgombea mmoja ambaye ni Eng. Hersi Ally Said, huku nafasi ya Makamu wa Rais ikiwaniwa na Arafat Ali Haji.
Aidha, jumla ya wagombea 16 wamejitokeza kuwania nafasi za Wajumbe, ambao ni:
Julius John Koyi
Saady Mohammed Khimji
Fredy Stanley Mahembe
Munir Said Seleman
Mshindo Hamza Msolla
Issa Ally Mangungu
Mustapha Salumu Himba
Alexander Francis Ngai
Gerald John Kihinga
Yanga Evarist Makaga
Fahd Ahmed Afif
Rodgers Hemedi Gumbo
Seif Khamis Gulumali
Mohamed Ally Mwenda
Mzee Yussuf Mwinyi
Prisca Josephate Kishamba
Orodha hiyo imetolewa rasmi na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga SC, ikiwa ni hatua muhimu kuelekea mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo.
