×

GSM Ampelekea Kombe Pacome Hospitalini Aga Khan Dar – Picha

Mdhamini na mfadhili wa Klabu ya Yanga SC, Ghalib Said Mohamed (GSM), amemtembelea kiungo wa timu hiyo, Pacome Zouzoua, baada ya kupata majeraha katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania.

Pacome alipata jeraha hilo katika mchezo wa jana uliochezwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, baada ya kugongana na mchezaji wa JKT Tanzania wakati wakigombea mpira, hali iliyomlazimu kuondolewa uwanjani kwa matibabu.

Katika ziara hiyo, GSM alionekana kumjulia hali mchezaji huyo na kumtakia nafuu ya haraka ili aweze kurejea tena uwanjani kuendelea na majukumu yake ya kuisaidia Yanga SC.

Hatua hiyo imepokelewa kwa pongezi kutoka kwa mashabiki wa Yanga na wadau wa soka nchini, wakieleza kuwa ni ishara ya kujali na mshikamano ndani ya klabu.

Yanga SC imeendelea kumhudumia mchezaji huyo huku ikifuatilia kwa karibu maendeleo ya matibabu yake, ikisubiri taarifa rasmi ya kitabibu kuhusu muda anaotarajiwa kuwa nje ya uwanja.

POLISI WAFICHUA WALICHOKIKUTA CHUMBANI GESTI ALIMOFIA DEREVA wa HECHE UCHUNGUZI WAENDELEA

Leave a Comment