×

Advela na Mama Yake Wamshukuru Shigongo kwa Kuwagharamia Matibabu ya Miguu – Video

Mtoto Advela pamoja na mama yake, Melisiana, wamemtembelea Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, kumshukuru kwa msaada alioutoa uliowezesha mtoto huyo kupata matibabu ya ulemavu wa miguu katika CCBRT, jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo imekuja miaka miwili baada ya kuanza kwa safari ya matibabu ya Advela, ambaye sasa ameonyesha maendeleo makubwa yaliyorejesha matumaini kwa familia yake.

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo (kushoto) akisalimiana na mtoto Advela baada ya kumtembelea kwenye ofisi yake jijini Dar es Salaam akiwa na mama yake.
Mtoto Advela amepata matibabu ya ulemavu wa miguu katika CCBRT, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Melisiana alisema msaada wa Shigongo ulikuwa wa thamani kubwa kwao kwani uliwapa nafasi ambayo hawakuwa na uwezo wa kuipata wenyewe. Alieleza kuwa matibabu aliyopatiwa Advela yameleta mabadiliko makubwa na kuifanya familia yao kuanza maisha yenye matumaini mapya.

Mtoto Advela pamoja na mama yake, Melisiana.

Kwa upande wake, Shigongo alisema jambo linalompa faraja zaidi ni kuona watu wanaopata changamoto za kiafya wakipata matibabu na kurejea katika maisha yao ya kawaida.

Alisisitiza kuwa kila anayepata uwezo wa kuwasaidia wengine anapaswa kufanya hivyo kwa moyo wa kujitolea, akisema baraka za mtu zina maana pale zinapotumika kuwainua wengine.

Shigongo pia aliwapongeza madaktari na wataalamu wa CCBRT kwa juhudi zao za kitaalamu zilizowezesha Advela kupata matibabu yenye mafanikio na kuanza maisha mapya.

Leave a Comment