
Mwili wa aliyekuwa dereva wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, Suez Dani Maradufu, umekabidhiwa kwa ndugu na viongozi wa chama hicho jioni ya leo kabla ya kuanza safari ya kuelekea wilayani Tarime, mkoani Mara kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.
Baada ya kukabidhiwa kwa familia na uongozi wa CHADEMA, ibada fupi ya kumuombea marehemu imefanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Kigoma, Maweni, ambapo viongozi, ndugu, jamaa na wananchi walijitokeza kutoa heshima zao za mwisho.
Baada ya ibada hiyo, mwili wa marehemu uliondoka Hospitali ya Maweni ukielekea Tarime, ambako familia itaendelea na taratibu za mazishi kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa.
Marehemu Suez Dani Maradufu anakumbukwa kwa huduma yake kama dereva katika ofisi ya uongozi wa chama, ambapo alihudumu kwa ukaribu na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA katika majukumu yake ya kila siku.

