
Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Prince Dube, amekamilisha rasmi uhamisho wake na kujiunga na klabu ya Hardrock FC baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.
Dube amejiunga na klabu hiyo kufuatia kumalizika kwa mkataba wake na Yanga SC, ambako alikuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kabla ya kurejea nchini kwao Zimbabwe.
Hardrock FC ni miongoni mwa klabu zilizopanda daraja kuelekea Ligi Kuu ya Zimbabwe kwa msimu ujao, na inatajwa kuwa na mipango mikubwa ya maendeleo ikiwemo miundombinu bora na uwanja wake binafsi.
Kwa mujibu wa taarifa za klabu hiyo, picha iliyotolewa inaonyesha Dube akiwa pamoja na mmiliki wa Hardrock FC mara baada ya kukamilisha rasmi usajili wake, ishara ya kuanza kwa safari mpya ya mshambuliaji huyo katika soka la nyumbani kwake Zimbabwe.
Uhamisho huo unamaliza rasmi kipindi chake akiwa na Yanga SC, ambapo alichangia kwa kiwango kikubwa katika safu ya ushambuliaji kabla ya kuamua kurejea katika Ligi Kuu ya Zimbabwe.