×

Mwana FA Aimba na Mashabiki Katika Maadhimisho ya Miaka 30 ya Bongo Fleva

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, ameshiriki tamasha la kihistoria la maadhimisho ya miaka 30 ya muziki wa Bongo Fleva, lililofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa wasanii wa vizazi mbalimbali waliotoa mchango mkubwa katika ukuaji wa muziki wa Bongo Fleva tangu ulipoanza hadi kufikia mafanikio ya sasa. Nyimbo zilizowahi kutamba katika vipindi tofauti zilitumbuizwa, zikiamsha kumbukumbu na hisia kwa maelfu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia maadhimisho hayo.

Katika kuongeza shamrashamra za tamasha hilo, Mwinjuma, ambaye pia ni mmoja wa wasanii waliowahi kutamba katika muziki wa Bongo Fleva, aliungana na wasanii na mashabiki kuimba na kucheza baadhi ya nyimbo zilizoweka historia katika tasnia hiyo.

Maadhimisho hayo yamekuwa sehemu ya kutambua mchango wa wasanii, watayarishaji wa muziki na wadau wengine waliochangia kukuza na kuitangaza Bongo Fleva ndani na nje ya Tanzania kwa kipindi cha miaka 30.

 

 

Leave a Comment