×

Malkia wa Olimpiki Simone Biles Aangaza ESPY kwa Gauni la Kipekee

Bingwa wa mazoezi ya viungo duniani na mshindi wa medali nyingi za dhahabu za Olimpiki, Simone Biles usiku wa kuamkia leo Julai 16, 2026 ameonyesha tena mvuto wake nje ya uwanja baada ya kung’ara kwenye zulia jekundu la Tuzo za ESPY 2026 zilizofanyika Julai 15 jijini New York.

Biles aliwasili kwenye hafla hiyo akiwa ameambatana na mumewe, mchezaji wa NFL Jonathan Owens, huku akivutia macho ya wengi kwa gauni la kifahari la rangi ya dhahabu lisilo na mikono. Gauni hilo lilikuwa na muundo wa kisasa wenye sehemu ya mbele fupi na mkia mrefu uliogusa sakafu, jambo lililoongeza uzuri wa mwonekano wake.

Ili kukamilisha mtindo huo, Biles alivaa mapambo ya almasi yaliyohusisha mkufu, hereni na pete, sambamba na viatu vya kisigino vya wazi mbele. Nywele zake zilikuwa zimepangwa kwa mtindo wa mawimbi na kugawanywa upande mmoja.

Mbali na kuzungumziwa kwa mavazi yake, Biles amekuwa akiwafurahisha mashabiki kwa kufichua baadhi ya mambo ya maisha yake binafsi. Kupitia video aliyowahi kushiriki kwenye TikTok, alisema alipokuwa mtoto alidhani ni watu wenye jina la Adam pekee waliokuwa na Adam’s apple.

Pia alifichua kuwa amewahi kufanyiwa upasuaji wa urembo mara tatu, huku akieleza kuwa upasuaji mbili kati ya hizo ni vigumu mtu kuzitambua. Aidha, alisema hakuwahi kufua nguo zake mwenyewe wala kutumia mashine ya kuosha vyombo hadi alipoanza kuishi peke yake.

Biles aliongeza kuwa mchezo wa mazoezi ya viungo ndiyo mchezo wa kwanza na pekee aliowahi kuucheza, na kwamba ana mzio wa aina kadhaa za lip gloss. Pia alisema hakukua akitazama filamu, jambo lililomfanya ashindwe kutazama filamu maarufu kama The Wizard of Oz na Forrest Gump.

Biles na Owens walifunga ndoa mwaka 2023 na wameendelea kuwa miongoni mwa wanandoa wanaovutia zaidi katika ulimwengu wa michezo.

Leave a Comment