
Subira imekwisha! Mashabiki wa soka wanakaribishwa kushuhudia Fainali ya FIFA World Cup 2026 kati ya Hispania na Argentina katika hafla maalum iliyoandaliwa na Oryx Energies.
Tukutane Mbagala Zakhem siku ya Jumapili, Julai 19, 2026, kwa burudani ya kipekee ya kutazama fainali hiyo kupitia screen kubwa, huku ukifurahia muziki kutoka kwa Live DJ, pamoja na vyakula na vinywaji vitakavyopatikana eneo la tukio.
Kinachofanya tukio hili kuwa la kipekee zaidi ni kwamba hakuna kiingilio. Ni nafasi kwa mashabiki wa soka kukutana sehemu moja, kushangilia, kupiga kelele na kufurahia mchezo mkubwa zaidi wa soka duniani.
Usikose kuwa sehemu ya historia ya fainali hii. Waite marafiki zako, familia na wapenzi wa soka mkutane Mbagala Zakhem tuushuhudie pamoja usiku wa mabingwa.
📍 Mahali: Mbagala Zakhem
📅 Tarehe: Jumapili, 19 Julai 2026
🆓 Kiingilio: Bure kabisa
Twende tukashangilie pamoja! ⚽🏆