Mwanamitindo maarufu nchini, Fahyma, ambaye pia ni mzazi mwenza wa msanii wa Bongo Fleva na Mkurugenzi Mkuu wa Next Level Music, Rayvanny, ameibua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya mashabiki kumiminika kumsifia kutokana na muonekano wake na ubunifu wake katika mavazi.
Fahyma amekuwa akipokea pongezi nyingi kutoka kwa mashabiki mbalimbali ambao wameeleza kuvutiwa na namna anavyoweka pamoja mavazi yake, wakimtaja kama mmoja wa mastaa wanaojua zaidi masuala ya mitindo nchini.
Baadhi ya mashabiki wameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa Fahyma kwa sasa anastahili kutazamwa katika kiwango cha juu cha fashion, wakimtaja pamoja na mastaa wengine wakubwa wa mitindo akiwemo Hamisa Mobetto.

Katika maoni yaliyotolewa kwenye picha zake, mashabiki wamempa majina mbalimbali ya sifa kama “Queen of Fashion”, “Diva wa kweli” na “Best Dressed Tanzanian Celebrity”, wakieleza kuwa ana upekee katika uchaguzi wa mavazi na namna anavyojipambanua.
“Queen of fashion 🔥🔥🔥🙌❤️❤️❤️” aliandika mmoja wa mashabiki.
Mwingine aliongeza: “Best Dressed Tanzanian celebrity always ❤️😍.”

Mbali na kusifiwa kwa upande wa fashion, mashabiki pia wamempongeza Fahyma kwa uzuri wake, unyenyekevu na namna anavyoonekana kuwa mwanamke mwenye kujiamini.
“A real Diva ❤️😍”, “I love every detail, so clean and cute” na “Mother of two, fashionista” ni baadhi ya maoni yaliyoonekana kutoka kwa mashabiki wake.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Fahyma ameendelea kujenga jina lake katika ulimwengu wa mitindo, huku kila anaposhiriki picha mpya akivuta macho ya mashabiki na wapenzi wa fashion.
Umaarufu wake katika eneo la mitindo umeendelea kukua, huku wengi wakimtaja kuwa miongoni mwa wanawake wanaowakilisha vizuri tasnia ya fashion nchini Tanzania.

