×

Bakari Msimu Atua Simba kwa Mkataba wa Miaka Miwili Akitokea Coastal Union

Klabu ya Simba imemtambulisha rasmi winga kijana Bakari Msimu kuwa mchezaji wake mpya, akitokea Coastal Union ya Tanga kuelekea maandalizi ya msimu wa 2026/27.

Msimu, ambaye ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 18, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba, huku akionekana kuwa sehemu ya mkakati wa klabu hiyo wa kuwekeza kwa wachezaji vijana wenye vipaji.

Kwa usajili huo, Bakari Msimu anakuwa mchezaji wa tatu kutambulishwa rasmi na Simba katika dirisha hili la usajili, baada ya Kelvin Nadhon na Nathaniel Chilambo.

Ujio wake unatarajiwa kuongeza ushindani katika safu ya ushambuliaji ya Wekundu wa Msimbazi, ambao wanaendelea kujiimarisha kwa ajili ya mashindano ya ndani na kimataifa msimu ujao.

Leave a Comment