
Mabingwa wapya wa Kombe la Dunia 2026, Hispania, wamerudi kileleni mwa viwango vya ubora vya FIFA kwa upande wa timu za taifa za wanaume, huku Argentina ikishuka hadi nafasi ya pili.
Hispania ilifanikiwa kupanda tena nafasi ya kwanza baada ya kuifunga Argentina kwa bao 1-0 katika muda wa nyongeza kwenye fainali ya Kombe la Dunia iliyochezwa Jumapili, ushindi uliowapa taji la dunia na kuwaweka tena juu kwenye orodha ya FIFA kwa mara ya kwanza tangu Januari.
Timu ya kocha Luis de la Fuente imeacha rekodi nzuri baada ya kuonyesha ubora mkubwa katika michuano hiyo.
Ufaransa imeendelea kushika nafasi ya tatu, huku England ikiwa nafasi ya nne licha ya kufungwa na England kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya tatu.

Brazil imepanda hadi nafasi ya tano, wakati Morocco imeandika historia kwa kufikisha nafasi ya sita, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kufikiwa na taifa hilo katika viwango vya FIFA.
Ureno imeshuka nafasi mbili hadi ya saba baada ya kutolewa katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia. Ubelgiji imepanda hadi nafasi ya nane huku Uholanzi ikishuka hadi nafasi ya tisa.
Mexico imeingia kwenye 10 bora baada ya kupanda nafasi nne, huku Norway ikiwa timu iliyopanda zaidi kwa kuruka nafasi 12 hadi ya 19 baada ya kufika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia.

Kwa upande mwingine, Ujerumani imetoka kwenye 10 bora na kushuka hadi nafasi ya 12, nafasi moja mbele ya Croatia. Italia, ambayo haikufuzu Kombe la Dunia, imeshuka hadi nafasi ya 15.
Katika timu nyingine, Tunisia imekuwa taifa lililoshuka zaidi baada ya kuporomoka nafasi 12 hadi ya 57. Misri imepanda hadi nafasi ya 24, huku Paraguay ikipanda hadi nafasi ya 34 baada ya kufika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia.
Cape Verde imepanda hadi nafasi ya 64 baada ya kufika hatua ya 32 bora, ikiwa juu kidogo ya Ghana ambayo imepanda kwa nafasi nane.
Viwango 10 Bora vya FIFA Baada ya Kombe la Dunia 2026
- 🇪🇸 Hispania
- 🇦🇷 Argentina
- 🇫🇷 Ufaransa
- 🏴 England
- 🇧🇷 Brazil
- 🇲🇦 Morocco
- 🇵🇹 Ureno
- 🇧🇪 Ubelgiji
- 🇳🇱 Uholanzi
- 🇲🇽 Mexico