×

Meja Kunta Apoteza Baba Yake, Afariki Akiwa Hospitalini jijini Dar

Baba mzazi wa msanii wa muziki wa Singeli, Meja Kunta, amefariki dunia muda mfupi uliopita alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam.

Kifo hicho kinakuja siku chache baada ya Meja Kunta kuweka wazi kuwa baba yake alikuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), huku akiomba dua na msaada kwa ajili ya matibabu yake.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape familia, ndugu na marafiki nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu.

Leave a Comment