×

Infantino Atingisha Soka la Dunia, UEFA Yatoa Onyo Kali Kuhusu Kombe la Dunia

Mvutano mkubwa umeibuka ndani ya Shirikisho la Soka Duniani baada ya taarifa kudai kuwa Rais wa FIFA, Gianni Infantino, anapanga kuuza sehemu ya umiliki wa biashara ya Kombe la Dunia kwa wawekezaji binafsi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mpango huo unahusisha kuanzishwa kwa kampuni mpya chini ya FIFA, ambapo wawekezaji wa sekta binafsi watanunua hisa katika kampuni hiyo, hatua ambayo imezua upinzani mkubwa kutoka kwa viongozi wa soka barani Ulaya.

Inadaiwa kuwa UEFA imeitisha kikao cha dharura kujadili suala hilo, huku baadhi ya taarifa zikieleza kuwa kuna uwezekano wa mataifa ya Ulaya kutishia kususia michuano ya Kombe la Dunia ikiwa mpango huo utaendelea.

Katika taarifa yake, UEFA imeukosoa vikali mpango huo, ikisema umevuka mipaka inayokubalika katika uongozi wa mchezo wa soka.

Shirikisho hilo limesema pendekezo hilo “limevuka mstari” na kuwataka wadau wote wa soka duniani kuchukua hatua kulinda misingi ya mchezo.

UEFA ilihitimisha kwa kusisitiza kuwa “roho na utawala wa soka si mali zinazopaswa kuuzwa, hasa wakati hakuna uwazi kuhusu nani atafaidika kifedha.”

Iwapo mpango huo utaendelea, unaweza kuwa chanzo cha mgawanyiko mkubwa kati ya FIFA na UEFA, huku ukifungua mjadala mpya kuhusu mustakabali wa uendeshaji na umiliki wa michuano mikubwa zaidi ya soka duniani.

Leave a Comment