×

Kesi ya Uhaini ya Lissu Kuendelea Agosti 10 Hadi Septemba 7, 2026

Kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Tundu Lissu itaendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kuanzia Agosti 10 hadi Septemba 7, 2026.

Mwakilishi wa timu ya mawakili wanaomtetea Lissu, Wakili Hekima Mwasipu, amesema wamepokea barua kutoka mahakamani ikieleza kuwa kabla ya usikilizwaji wa shauri kuanza, kutafanyika kikao cha awali cha maandalizi mnamo Agosti 5, 2026.

Lissu alikamatwa Aprili 9, 2025 na kufunguliwa mashtaka ya uhaini. Usikilizwaji wa kesi hiyo ulisimama tangu Februari 24, 2026 baada ya kufunguliwa shauri la marejeo katika Mahakama ya Rufani, likihusu mwenendo wa kesi na uamuzi wa Mahakama Kuu wa kukataa kupokea ushahidi wa nyongeza kutoka kwa ACP Amini Mahamba.

Hatua hii inafuatia uamuzi wa Mahakama ya Rufani uliotolewa Julai 30, 2026, ambapo iliyatupilia mbali maombi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ya kutaka mapitio ya uamuzi wa Mahakama Kuu, hivyo kufungua njia kwa kesi hiyo kuendelea kusikilizwa.

Leave a Comment